Wednesday, September 6, 2017

DILAILAT AFUNGUKA KUHUSU VIDEO YA SAIDA KAROLI

Mwanadada anaechipukia kwenye mitindo ya uigizaji (model) maarufu kama @dilailat_taher  apata shavu baada ya kupendezesha Video ya wimbo wa Saida karoli (Kichaka) ft Belle9 & Gnako.

Amesema,...


Dilailat
























Tangu video hiyo kutoka leo ikiwa ina siku ya tatu mtandaoni, Mwanadada huyo ameweza kuonesha hisia zake na kutoa shukurani kwa Mwanamuziki Mkongwe Saida Karoli kwa kuweza kushiriki katika video hiyo kwa ilikuwa moja ya ndoto zake

"Namshukuru Sana Saida Karol amenifanya kwasasa  kuna baadhi ya wasanii wamenifahamu na kunitafuta kufanya kazi na mimi " 

alisema maneno hayo katika kumshukuru mwanamuziki huyo Mkongwe Saida Karoli 
Pia alimalizia na kusema kwamba hivi sasa anategemea kufanya kazi nyingi sana hivyo anawaomba watanzania wakae tayari kwa ujio wake.


Saida Karoli






Dilailat akiwa na Msanii G Nako kwenye Video mpya ya Saida Karoli