Sunday, May 12, 2013

RIYAMA ALLY ANAPENDWA NA YUSTER!

Mwanadada Yuster Mwakachara ni Msanii anaekuja kwa kasi katika Tasnia ya filamu Tanzania baada ya kuonekana katika kazi nyingi akiwa anafanya vizuri sana kama kwenye MWANAUME HULKA, SUBIANI, STOLEN GOLD n.k

Kwasasa Yuster yuko katika kuandaa filamu yake mpya ambayo hivi karibuni ameibuka na kusema kuwa anampenda sana Mwamama Riyama Ally ambae kwasasa ana Mtoto wa kike.

Yuster ameshafanya kazi moja nae katika filamu ya SUBIANI lakini bado anahisi kuwa kiu yake haijaisha katika kushirikiana na msanii huyo nguri wa kike kutokana na uwakilishaji wake mzuri katika sanaa yake.

Akiendelea na kusema kuwa katika wasanii wa kike Nchini Tanzania anafikiri na kudhani kuwa hakuna kama Riyama Ally hivyo inapotokea kuwa anafanya nae kazi anajikuta akiwa na juhudi ya ziada katika kuhakikisha anafanya vizuri bila kumuangusha mtu yeyote katika upande wake.