Sunday, May 12, 2013

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WASANII

 Mheshimiwa Waziri Mkuu Mzengo Pinda ambae alikuwa mgeni rasmi katika mkutano ya Wasanii katika kutetea haki zao uliofanyika Jijini Dodoma, amekuwa msatari wa mbele katika kuwaunga mkono wasanii hao katika zoezi lao hilo na kuhakikisha kuwa wanapata haki zao na kusimamiwa vyema kwa kazi wazifanyazo.

Katika Mkutano huo wasanii wengi wameonekana kuhamasika huku wakiwa wanaonesha umoja na mshikamano juu ya suala hilo.

Kimekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wasanii kuibiwa na kudhulumiwa kazi zao hivyo kwasasa ni mfano wa matumani mapya ambayo yameingia katika sehemu iliyokumbwa na majanga ambayo yaliweza kuteketeza wengi waliokuwa wameanza lakini hawakupata mafanikio kutokana na kazi yao ya sanaa.

Ni wazi kwasasa kwa wasanii kuonesha ushikiano bila kuangalia nani ni nani ili kutoa nguvu zao katika zoezi hilo kwa pamoja.