Sasa kitu kichafu huenda kikaonekana si cha kuweza kupikwa, lakini ni kitu ambacho kinavutia katika maeneo mengi ya hapa barani kwetu Afrika - hasa miongoni mwa akina mama wajawazito wanaohitaji virutubisho vilivyomo ndani ya udongo.
Hapa kwetu Nchini Tanzania kuna udongo maalum unaojulikana kwa jina la udongo wa pemba.
Tulanana Bohela amesafiri hadi katika vilima vya vya Morogoro kujua udongo huo una ladha gani, lakini safari yake aliianzia katika soko maarufu la Kariakoo Dar Es Salaam.