Friday, October 25, 2013

IRENE UWOYA AMPIGA CHUPA YA BEGA RAY USIKU WA SAA 6.

Vicent Kigoso wengi wamezoea kwa jina la Ray ni msaani mahiri katika tasnia ya filamu Tanzania na Africa mashariki, jana usiku majira ya saa 6 akiwa maeneo ya jirani na kwao anapoishi alionekana akiwa anaamua ugomvi mkubwa uliotokea usiku huo baada ya mwanamama Irene Uwoya kusikia akiwa anatukana sana kwa kulalamika kuwa, kuna mtu ambae anamuharibia maisha yake, mbali na hayo inasemekana Irene Uwoya aliweza kurusha chupa na kupata Ray kwa bahati mbaya lakini haikuweza kuvunjika ila haikuweza kumjeruhi.
Sakata hilo lilichukua muda takribani dakika 30 mpaka kupatikana kwa maelewano baada ya Vicent Kigosi "ray" kumuita mmoja wapo ili kuweza kusuluhisha ugomvi huo na kumuomba sana Irene ajaribu kutulia.
Kwa sauti ya juu Ray alisikika akiita mtu ambae alijulikana kwa jina la "Mnyama" ili aweze kufika pale na kiyamaliza huku Ray akiwa anamwambia Mnyama apige nagoti na kumuomba msamaha Mwanamama huyo mrembo Irene Uwoya...patamu hapo...Mnyama aliweza kupiga magoti na kuomba msamaha.
Haikuweza kufahamika rahisi hasa tatizo ilikuwa ni nini ila kulikuwa na kukosekana kwa maelewano baina ya Irene Uwoya na mwenzie Mnyama ambao watu hao wawili wana mahusiano ya kimapenzi.
Baada ya muda zilisikika sauti za vicheko na watu wakawa wanaendelea kula bata kama kawa.

Hongera Vicent Kigosi kwa ku-show love kwa watu wako...








Hongera Vicent Kigosi kwa ku-show love kwa watu wako.