Sunday, May 12, 2013

JE UNAJUA SABABU YA MRISHO MPOTO KUTEMBEA PEKU (BILA VIATU) ?

Msanii gwiji katika muziki wa asili ambao una mashahiri mazito na yenye misemo mkali sana ambayo hupelekea kuwagusa watu mbalimbali katika jamii hadi Serikalini kwa kile anachokizungumzia kila siku kwenye mashairi yake hayo hapa tunamzungumzia Mrisho Mpoto.
Hii ni habari za kawaida tu kutokana na mabadiliko mbalimbali ya wasanii pale walipoanza na kufikia hapa katika daraja fulani la mafanikio yao pia nadhani kutakuwa na maswali mengi watu watajiuliza kwa hiki ambacho leo nitakizungumzia hapa.
Kwanini Msanii huyu hupenda kutembea bila viatu (peku) akiwa katika show zake pia
inasemekana hata katika mazingira ya kawaida anapokwenda kufanya mahojiano na waandishi wa habari mbalimbali, Je nini sababu ya kumfanya awe anatembea peku?
Mimi sijui, ila katika uchunguzi wangu nikajikuta niliona hili kwa kina zaidi ukija kuangalia hapo mwanzo hakuwa na wazo la kutembea peku nadhani kwake angeona kama kujifedhesha mbele za watu na kuonekana kama kihoja kwa upande mwengine labda alikuwa anawaza atoke vipi ili aweze kuwapata ma-fans wake nae.
Hii ni changamoto kwa wote tunapaswa kujiuliza jamani, sitaki kusema ni ushirikina unatumika la hasha hizo ni hisia ambazo zitakuwa katika moyo wako baada ya kuisoma nakala hii.

Mrisho Mpoto ni msanii ambae yuko juu kwasasa na wenye kufikia level za Kimataifa katika muziki wake huo huku akiwa anaitangaza Lugha yetu vile ipasavyo amekuwa akikubalika na rika lote pale anapofikisha ujumbe na mtindo wake huo kama anaongea.

Wanajamii, Mashirika mbalimbali na Serikali imekuwa ikimtumia pia katika kazi za kijamii kutokana na sanaa yake ya kueleweka zaidi na mwenye kuigusa jamii nzima.

Haya basi caimani jibu tutakuja kulipata na kufahamu kwa kina zaidi siku tutakapobahatika kukaa nae pamoja na kufanya nae maongezi kwa kina.