Tuesday, December 10, 2013

HABARI ZA MZEE SMALL ZAZUA UTATA...

Baada ya habari Mzee Small msanii wa maigizo Nchini Tanzania kusambaa katika mtandao wa kijamii huku bila kuwa na uhakika wowote wa suala hilo na kupata vidokezo kwenye bolgs tofauti, Leo hii asubuhi nimepata taarifa kuwa Mzee inasemekana yuko hai na hakuna habari zozote ambazo zinahusiana na kufariki kwa Mzee huyo.

Taarifa ambazo zimekuwa zikizagaa katika mtandao huo wa kijamii Facebook imepelekea wengi kuamini na wengine kujiuliza maswali mengi kwa kutoamini na kuendelea kuuliza maswali mengi juu ya kutaka kupata uhakika wa kutosha.

Taarifa kwamba mwigizaji wa bongo movie Mzee Small amefariki nilizipata kwenye mida ya saa sita usiku na ni taarifa ambazo wengi waliziamini kutokana na ukweli kwamba mzee huyu amekua akiripotiwa kuugua kwa muda mrefu.
Breki yangu ya kwanza ilikua ni Amana Hospitali saa saba na dakika kumi usiku ambako sikukuta chochote au dalili hata za Wasanii au wahusika wa msiba kuwepo maeneo ya hospitali kama ambavyo huwa ni kawaida, badala yake nilikutana na baadhi ya wahudumu wa hospitali ambao japo sio wasemaji, walikiri kwamba Mzee Small wanamjua na kifo chake hakipo kwenye hospitali yao kama taarifa ilivyosambaa.
Baada ya hapo breki yangu ya pili ilikua nyumbani kwa Mzee Small mwenyewe Tabata ambako kiukweli hakukuwa na mazingira yoyote ya msiba kama ilivyo kawaida kwamba lazima ukute tayari watu wameanza kukusanyika, kulikua kimya na watu walikua wamelala.

Wakati huohuo nikiwa Tabata nilikutana na mmoja wa waigizaji na pia muandaaji wa movie za Comedy ambae alikua wa kwanza kufika nyumbani kwa mzee huyo saa moja iliyopita kabla ya mimi kufika, anasema ‘Niligonga kwa Mzee Small lakini hawakufungua kwa sababu ilikua usiku, walihofia usalama ila Mke wake kwa dirishani akaniambia Mzee Small ni mzima na amepumzika ndani, maneno hayohayo aliniambia mtoto wake wa kiume kwa dirishani na sikuona pilikapilika zozote za msiba.. yani maisha yako kawaida’
Taarifa nyingine ni kwamba kuna mzee mfupi aliekua akiishi Tabata pia na jina lake jingine anaitwa Mzee Small ndio kafariki, sasa watu ndio wamechanganya wakidhani ni Mzee Small Mchekeshaji.

Asante sana Kaka
-Millardayo