Mwanamitindo Nchini Tanzania Lotta Mollel azidi kufanya vizuri katika tasnia hiyo ya mitindo hapa nchini baada ya kuchukua tuzo nyingene tena ya BEST MALE MODEL katika maonesho SWAHILI FASHION WEEK huku ukiachilia lile shindano la kumtafuta Mr Tanzania 2013-14 ambalo aliweza kufanya vizuri sana na kumuweka katika sehemu nzuri.
Kwa kiasi kikubwa Lota Mollel ameonekana kukosa upinzani katika tasnia huyo kwa mwaka huu na kuwa kinara na kufanikiwa kuchukua Tuzo mbili kubwa katika mashindano hayo ambayo yaliweza kufanyika miezi hii ya karibu.
Kwa sasa Lotta Mollel yuko katika maandalizi makubwa sana kwaajili ya kuelekea Nchini Lagos Nigeria kwenye mashindano hayo makubwa ya kumtafuta Mr Africa mwakani mwezi January.
Watanzani na wadau wote ni vyema na ni wakati muafaka wa kuweza kuonesha uzalendo katika tasnia hii na kumpa nguvu ya kutosha Lotta mollel ili kuweza kuipandisha Bendera Tanzania kule Nchini Lagos Nigeria na kutuwakilisha vizuri katika shindano hilo la Kimataifa, tuahitajika kutoa mchango mkubwa sana kwa Mwanamitindo huyu ili kuweza kufanikisha ushindi na kurudi na Tuzo hiyo ya MR AFRICAN.
Unaweza kumcheki kwenye Facebook kwa lolote lile kama mdau wake.

