Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Recho, Fid Q, Ney wa Mitego, Madee, Stamina na Roma Mkatoliki waliacha gumzo mkoani Morogoro kufuatia shoo ya nguvu waliyofanya katika tamasha la uzinduzi wa Huduma ya simu katika kampuni moja ya simu hapa nchini lililofanyika wikiendi.
Recho ambaye hivi sasa anatamba na wimbo wake mkali wa 'Mwali Kigego', ambao umezifuatia nyimbo zake za 'Kizunguzungu' na 'Upepo', aliwaacha hoi mashabiki wakati alipotumbuiza huku akinengua.
Rapa Fid Q alipagawisha kwa ngoma zake kali kama ilivyokuwa kwa Ney wa Mitego ambaye anatamba hivi sasa na wimbo wake wa "Muziki Gani' aliourekodi kwa kumshirikisha Diamond Platnumz.
Wasanii wengi waliowapeleka puta mashabiki wa Morogoro walikuwa ni Madee aliyepagawisha kupitia nyimbo zake kali kama "(Nani Kamwaga) Pombe Yangu" huku Stamina akiimba "Wazo la Leo" alioimba na Fid Q.
Huku wakiimba nyimbo zao, wasanii hao pia walikuwa wakiitumia fursa yao jukwaani kutangaza huduma za kampuni ya simu.
Ofisa wa Mtandao, Alex Msigara alisema alisema lengo la onyesho hilo lilikuwa ni kutambulisha huduma za simu ya kampuni hiyo ya simu