Bila kujali usalama wa maisha yao kuanzia mteja aliepakia katika hiyo Bodaboda mpaka dereva mwenyewe kwa mtindo ambao wameamua kukaa katika chombo hiko.
Hakuna hatari ambayo wameweza kuifikiria katika maisha yao bali wanachowaza kufika na mizigo walio nayo kama inavyonekana huku abiria akiwa amekaa juu ya matairi yake huku akifurahi kuonesha ameridhika na hali hiyo, kwa
kweli mwendo ulikuwa mkali sana kwa kiwango

Watu hao ambao hawakufahamika kwa majina waliweza kujitambua kuwa wanapigwa picha na mpiga picha wetu lakini hawakuweza kujali kwao ilikuwa kama starehe huku wakiwa wanazidi kuongeza mwendo.

Wingi wa ajali za Bodaboda barabarani husababishwa na uzembe kama huu, kwasababu mtu anashindwa kujali na kufata sheria za barabarani na kuendesha chombo hiko katika mazingira hatarishi nakwa upande mwengine kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Askari wa Usalama barabarani lakini bado limekuwa tatizo sugu kwa hawa madereva wa Bodaboda.
Kama hali hii itaendelea bila kuangaliwa kwa makini zaidi na kutafutiwa ufumbuzi hajali hazitapungua na watu watakatika miguu kila siku na wengine kupoteza maisha kwa matumizi ya hiko chombo.
Samaki mmoja akioza huwa tunaelewa wote nikiwa na maana kwamba kuna madereva wazuri wa bodaboda lakini huchafuliwa na kuonekana hawana maana kwa kosa la Dereva huyu mmoja.
Najua madereva wa Bodaboda wana umoja wao kama pale inapotokea mwenzao akipata ajali au kugongwa huwa wana ushirikiano wa kutosha.
Je kwa huyu anaevunja Sheria wanamfanyaje?
TULIANGALIA HILI KWA MAKINI.