Monday, December 24, 2012

MSANII WA BONGOFLAVA AINGIA MITINI!!


MOST WANTED

Ni msanii chipukizi wa muziki Bongoflava Yusuph Amr a.k.a Uzeal Brighter kutokea shinyanga pia ni mfanyakazi katika kampuni moja ya simu hapa nchini VODACOM huko huko shinyanga anatafutwa kwa kesi ya madai baada ya kufanyiwa video na kampuni ambayo iko Dar Es salaam PLAN B SOLUTION LTD.
Kijana huyo alitoka shinyanga kuja Dar Es Salaam kwaajili ya kufanya video ya wimbo wake ambao unakwenda kwa jina la "Natafuta" baada ya kuona kazi yake imekamilika aliweza kuondoka katika ofisi hizo na kuahidi anakwenda kuchukua pesa na huo ndio ulikuwa mwanzo wa kuwa na maisha magumu ya kuzima simu na kutopokea simu anazopigiwa inafika sasa mwezi.
Director wa Video hiyo alikuwa na haya ya kusema...
"Ah huyu msanii kiukweli nilifahamishwa kwake na rafiki yangu mmoja hivi so nilitokea kumuamini kutokana na jamaa na kwa jinsi nilivyoona ametoka mbali kwaajili ya kuja kufanya video nikaona sio tabu, wala sikuyafikiria kama haya yangetokea ila namdai pesa nyingi kwasababu niliyumia gharama zangu baadhi ya vitu, muda pamoja na nguvu yangu na sijaishia hapo ila taarifa zimeshafika mahala husika na zinashughulikiwa mi nafikiri nifate sheria tu sihitaji matatizo na mtu, alichofanya sio poa kabisa, istoshe mpaka Video model wangu hajamlipa dah! ATAISOMA MZAZI

Ila Director huyo hakutaka kutajwa jina lake kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake, tutaendelea kufatilia ishu hii mpaka tutakapo jua tamati yake ni nini!