FARID UWEZO
Ni kijana mwenye jina kubwa tu katika Tasnia ya Filamu Tanzania kwenye upande wa kupiga picha na kuhariri kazi za filamu Farid Uwezo ambae maskani yake Magomeni Moroko hoteli.
Ana rekodi ya kufanya filamu nyingi sana za hapa kwetu Tanzania na wasanii mbalimbali wakubwa Vicent Kigosi "Ray", Jackline Wolper, JB, Haji Adam, Steve Nyerere na wengine wengi na hadi wachanga katika hii Tasnia pia kwa sasa ameanzisha kikundi chake cha Sanaa kinachoitwa Owes Artist Group kilichopo hapo hapo karibu na ofisi na TAF nia na malengo yake ni kuinua vipaji vipya.
Tulipokaa na Farid Uwezo ingawa tuliongea mengi lakini dondoo yake kubwa kwa mwaka huu ni hii..
"Nashukuru mpaka sasa nimefanya filamu nyingi sana pia naendelea kujifunza vitu vipya kupitia hii kazi yangu na nawashukuru sana Watanzania na Wasanii kwa ujumla kwa kukubali kazi zangu na kuonesha ushirikiano naaaa... ila kuhusu suala zima la mahusiano mzeee, Arbab hapo bado siko tayari kwasababu maadili ya kwetu hayaturusu ila muda ukifika nitaweka bayana kwa kufanya tendo lenye kuhitajika moja kwa moja kama ni kuoa au vipi, Napenda kuwatakia Heri ya Krismas na mwaka mpya Watanzania na Afrika Mashariki wote"
Haya muda ukifika ataweka bayana mi hapo sina neno jamani!

