Rais wa zamani wa Afrika Kusini
ameaga dunia . Mandela ameaga akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye
aliongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa enzi ya ubaguzi
wa rangi nchini Afrika Kusini baada ya kufungwa jela kwa miaka 27
Mandela alikua anpokea matibabu ya homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.Mnamo mwaka 2005, Mandela alitangaza kwa taifa kua mwanawe wa kume alifariki kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kuondoka gerezani.
Hakuonekana sana hadharani tangi alipostaafu mwaka 2004.



