Monday, May 20, 2013

G. NAKO LIVE 100%

Ndani ya New Maisha Club usiku wa jana Jumapili G. Nako rapa kutokea A Town "Arusha" akiwa pamoja na timu yake nzima ya WEUSI wakimsindikiza vyema katika show yake hiyo hapo jana.

G. Nako jana alikuwa anatambulisha video yake mpya ya MAMA YEYOO ambayo amefanyia kwao Arusha huku akiwa ameshirikiana na Msanii wa kizazi kipya BEN PO katika track hiyo.

Katika utambulisho wa video yake mpya hapo jana, G. Nako aliweza kupata support kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao walioweza kuisindikiza vizuri show hiyo ukiachilia timu yake ya WEUSI akiwemo BEN PO, BARNABA, PETER MSECHU, DAMIAN na wasanii wengine wengi tu.

G. Nako aliamua siku hiyo kubadilisha muziki wa bongo fleva kwa kufanya LIve Band kwenye stage na kupiga show kwa muda mrefu na wapenzi wa muziki huo bila kuchoka mpaka kufikia kumalizika kwa show.
Ilikuwa changamoto kwa wasanii wengine siku hiyo katika kufanya muziki wa Live lakini mambo yaliweza kwenda vizuri hakuna kilichoharibika kwa siku hiyi, mbali na hapo imekuwa ni somo kwa wasanii wengine kutokana na kukutana na changamoto hiyo ya muziki wa live.

Imezoeleka na ni kama kasumba ambayo imewatawala sana wapenzi wa muziki wa kizazi kuupenda muziki wa PLAYBACK kutokana na wasanii kulazimisha kufanya hivyo kutokana na uwezo mdogo wa kutumia au kufuata vyombo wanapokuwa jukwaani.

Lakini jana imekuwa tofauti kwa Rapa G. Nako na kufanikiwa kuteka hisia za mashabiki wa Muziki huo na kuupokea vyema kwa kitendo cha kufanya Live jukwaani, G. Nak alionekana ni msanii mwenye uwezo mkubwa na katika jukwaa kwenda sambamba na vyombo huku mashabiki wakiwa wanaendelea kushangilia bila kuchoka.