SALIM MLINDILA a.ka. Dream kijana ambae anachipukia kwa kasi katika muziki wa kizazi kipya BONGO FLEVA amekuwa ni gumzo sasa kwa Wasanii wengi wa Luninga katika Tasnia ya filamu Tanzania "BONGO MOVIE" baada ya kufanya wimbo ambao umekuwa ukitumika kama Sound track ya filamu hiyo ijulikanayo kwa jina la SINDANO YA MOTO ambayo inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.
Hali hiyo imekuwa ikiwatia sana hamu wasanii wengi sana katika Bongo movie kutamani kufanya kazi na kijana huyo katika kuandika na kutengeza nyimbo mbalimbali kwaajili ya filamu zao.
Msanii mahiri katikaTasnia ya filamu SULEIMAN BARAFU ni kati ya wasanii ambao waliokuwa wa mwanzoni katika kumsikia kijana huyo nakutamani na kazi ambayo alioifanya na kuamini kuwa haijawahi kutokea na kama iliwahi kutokea basi haikuwa kama hii, kwasababu hii imechukua hisia zote za filamu husika bila kuacha kitu chochote na anaamini kuwa ni filamu ya kwanza Tanzania ambayo itakuwa imechukua asilimia 85% za uhalisia wa kutosha na tofauti kama tulivyokuwatunategemea.
Gwiji huyo alimaliza na kusema "Natamani sikumoja nikamuona kijana huyu na kumueleza nia yangu ya kufanaya na kazi muda wowote kuanzia sasa maana amenipa ambayo nilikuwa nikiwaza muda mrefu lakini sikupata mtu ambae angenipa hisia za kutosha kama alichofanya kijana huyu, kiukweli nahitaji kufanya nae kazi kwa gharama zozote tutakazokubaliana"
Bado maswali mengi wasanii wengi wa Bongo movie wamekuwa wakijiuliza maswali kwa kitu ambacho kimefanyika katika wimbo huu ambao mpaka sasa tayari pia video yake ikiwa imeshakamilika bado kuachiwa, Ni wimbo ambao umetokea kupendwa na wengi kwa muda mufupi
kiasi ambacho wanatamani kuiona hiyo filamu ambayo ilitengenezewa filamu hiyo husika ilioandalia chini ya kampuni ya PLAN B SOLUTIONS.
Baadae aliweza kujitokeza Msanii mwingine wa kike maarufu sana na kipenzi cha wanawake katika sanaa yake aliokuwa nayo NDUMBANGWE MISAYO a.k.a THEA ambae nae anahusika vizuri tu katika filamu hii hivyo imekuwa ni mshangao mkubwa sana kwake baada ya kusikia habari hizo na kuongea haya.
"Haah we naamini itakuwa nzuri sana kwasababu kwa taarifa ninazosikia si kawaida pia natamani sana kumisikia huyo kijana naimani naweza kufanya nae kazi kiukweli"
Hizo ndizo habari ambazo zimekuwa zikiwafanya wasanii wa Bongo movie kupata matamanio na kuamua kumsaka kijana huyo kila kona kwa udi na uvumba kwaajili ya kutaka kufanya nae kazi.
Kwasasa Dream yuko katika kuandaa kazi yake mpya katika Studio ya NATAL Recods iliyopo Mburahati kwa lengo la kuwadhihirishia Watanzania na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kuwa amekuja kwaajili ya kuleta changamoto kwa wengine.
Alimaliza na kusema "Sikuamini na wala sikutegemea kama huu wimbo ungekuwa ni gumzo kiasi hiki ila niliamini kuwa naweza na nitafanya kitu kizuri kwahiyo imekuwa mara mbili zaidi ya vile nilivyokuwa nafikiria, namshukuru na Mungu na Watu kuweza kunikubali kwa kazi yangu na namaliza na kusema tuko pamoja niko tayakufanya kazi na yeyote atakekuwa tayari, sina tabu! Asanteni kwa kunipa support"
Endelea kufuatilia......