Tuesday, January 1, 2013

SAJUKI AFARIKI DUNIA!!!!


Msanii Juma Kilowoko (SAJUKI) amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu

Sajuki ambavyo kama anavyojulikana na wengi kwa sinema zake za kashkash alikuwa akiugua maradhi ya muda mrefu mpaka kufikia stage ya kupelekwa india kwa matibabu zaidi

Sajuki ambaye ameacha mjane ambaye pia ni msanii aitwaye wastara ambaye ni mlemavu wa mguu mmoja ambao ulisababishwa kwa kupata ajalii mnamo mwaka 2008 siku chache kabla y ndoa

Hata hivyo sajuki aliamua kumuoa hivyo hivyo kwani alikuwa ameshapeleka posa kwa kina wastara

Tukio hilo liligusa hisia za watu wengi na kumchukulia sajuki kama shujaa na mwanaume mwenye mapenzi ya kweli kwa kitendo hicho alichokifanya

Mwaka 2011 haukua mzuri kwa sajuki kwank ndio mwaka ambao maradhi yaliyomsumbua muda mrefu yalipamba moto

Inajulikana kuwa sajuki aliumwa na kufikia kipindi cha kudhoofu mwili wake kitu kilichopelekea wasanii wenzake na watu wengine waanzishe mchango wa kumchangia sajuki

Waasanii, wanasiasa, wananchi walifanikisha zoezi hilo na kumfanya aweze kwenda india kwa matibabu zaidi.

Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta nyuso za furaha na amani miongoni mwa watanzania

Hata hivyo alikuwa hajapona sawa sawa na alikuwa anajiandaa kurudi tena india kwa matibabu zaidi.. na hii alikiri kwenye kipindi cha mkasi

Sajuki ambaye ni mngoni ameshacheza maigizo na filamu na wasanii wengi karibia wote wenye majina hapa tanzania

Sajuki ambaye kwa kusaidiana na mkewe walifungu kampuni ya productions kwa ajilinya movies za hapa hapa nchini tanzania

Bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake lihimidiwe