Monday, December 24, 2012

WALIKUWA WANAFANYA NINI?


HAPA MI SINA NENO!
Haya ndio mambo ya kizungu au? Hili ni swali ambalo najiuliza mimi sijui wewe utajiuliza swali gani kama sio moja basi ni mengi na yataleta hoja pia.
Wanafahamika sana katika Tasnia ya Filamu Tanzania kwa majina ni nje ya uwezo wangu kuyaweka kwasababu maadili yangu hayaniruhusu kufanya hivyo, waswahili wanasema mtu kidole na kama hujui kusoma basi hata picha! hayo ni maneno ya kwetu sisi waswahili sasa tukija katika dondoo ya msingi kabisa ambayo inatuweka hapa.

JE SANAA NI UHUNI? JE MAFUNZO GANI AMBAYO WANAPATA JAMII KUPITIA HAWA WASANII WETU?

Tunasema kuwa Samaki mmoja akihoza basi wengine ni ngumu kunusurika sasa basi,
JE WENGINE MNAKUBALI KUNIKIA HARUFU YA MZOGA?
Ukishanukia harufu ya mzoga nani unafikiri atapenda kukaa na wewe...?
Tunawategemea sana Wasanii wetu wa hapa katika kuielimisha jamii kwa namna moja au nyingie na pia tunawaheshimu sana katika hiyo kazi na ndio maana kwa kipindi hiki kazi za kwetu zimekuwa zikitazamwa kwa kiasi kikubwa sana tofauti na zamani na hii inatokana na juhudi zenu na kazi zenu nzuri lakini inakuwa tofauti mkiwa katika mazingira ya kawaida.

"HAIPENDEZI KWA VIOO VYA JAMII"