Sunday, December 16, 2012

Sasa tupo katika mchakato mzima wa kuweza kukamilisha Filamu fupi ya dakika 4 iitwayo MASUMBUKO....

MASUMBUKO 
Kwenye kazi hapakosi misukosuko, yawezekana ikawa ajali kazini, akili kuchoka sana yote tisa inategemea unafanya kazi katika mazingira gani.
Asilimia kubwa katika Tasnia ya Filamu Tanzania huwa tunafanya kazi katika mazingira magumu sana , nikiwa na maana kwamba ukizingatia watendaji wa kazi ambao hutakiwa kuwa nyuma ya kamera hawajitoshelezi na pia wengi wao hawana elimu na uzoefu wa kazi hiyo hivyo Muongozaji  "Director" wa kazi hiyo hutumia akili nyingi na nguvu kuzuia jahazi kutozama. Pili Ku-copy taaluma na ujuzi kwa kumuona mtu anavyofanya kazi nikiwa na maana elimu inaiitajika kwa kiasi kikubwa sana "TUSIKOPI NA KUPESTI" Najua Watanzania huwa tunatumia sana Vipaji na kusahau Elimu, ni sawa ila tukumbuke elimu una nafasi kubwa sana katika kazi yeyote......
Watanzania wenzangu tuliopo katika Tasnia ya Filamu tunapaswa kwenda Shule kuongeza maarifa katika vipaji tulivyonavyo......