KAZI NI KWAKO MWANAHARAKATI WA KWELI
"FANYA KWELI HIP HOP IDUMU"
KESHO NEW MAISHA CLUB!!!!!!!!
Ally Kasongo Ram, Ni Editor, Cameraman na Director katika kazi nzima ya BUM KUBAM! huku akishirikiana na Crew nzima ya PLAN B SOLUTION ikiongozwa na Chief Director SHARNEL DEO katika kusababisha mpango mzima wa Documentary ya BUM KUBAM mpaka inakamilika ikisimamiwa vyema na FICHUKA DEVELOPMENT AGENCY LTD kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa....
Haya ni machache kutoka kwa Ram
"Ni kweli hii imekuwa ni changamoto kwetu katika kufikiri kwa muda mrefu juu ya kudhibiti wizi wa kazi za wasanii lakini kwangu imekuwa kama surprise kwasababu sikuwa na wazo kama hili la kufanya kitu kikubwa katika kuokoa muziki wa Tanzania kwa wamiliki wa kazi zao kutoibiwa.
First time Director wa kampuni ya FICHUKA alipoku ofisini na kunikuta na mwenzangu baada ya kutueleza idea aliokuwa nayo I was very surprised actual hivyo sikusita kumwambia mwenzangu kuingia mzigoni na kufanya hiki hiko.
Documentary hii itakuwa ni changamoto kwa wasinii wengi wa hapa kwetu Tanzania kwasababu ni kitu kipya na kigeni kabisa katika kazi zao na ni sehemu ya kuanzishwa kwa muundo mpya wa uuzwaji wa kazi za wasanii fichuka.com
Pia napenda kutoa shukrani kwa wote ambao tumeweza kushirikiana mpaka zoezi hili linakamilika bila kuingiliwa na kikwazo chochote kile NIKKI II, G. NAKO, BONTA, LOTTA na wengine wengineo pia kwenye upande wa media CLOUDS TV na RADIO, DTV n.k"
Hii ni kwa niaba ya PLAN B SOLUTION LTD
