Mzee Msisiri ni Mzee hodari sana na Mashuhuri katika kazi yake ya sanaa ya uigizaji hapa Nchi Tanzania, mpaka kufikia hapa historia yake ni kubwa sana na amefanikiwa kucheza filamu nyingi sana na wasanii mbalimbali wa hapa nchini na pia katika kazi yake hiyo kitu kilichomfanya kuwa maarufu ni zile sehemu za uchawi na zenye kuchezewa katika mazingira ya kijijini.
Kwasasa ni Mzee ambae anafanya vizuri katika Tasnia ya Filamu Tanzania baada ya kushiriki katika filamu mpya ya MPALANGE ambayo imeingia sokoni kama miezi miwili iliopita na kumfanya awe gumzo katika ulimwengu huo wa sanaa ya maigizo.
Filamu za Kiasili huwa ni filamu ambazo zinafanya vizuri sana katika soko la Dunia hasa kutoka katika nchi za kwetu Afrika mfano Nigeri, Ghana, Tanzania n.k lakini kwa Nchini kwetu bado tumekuwa na kasumba ya kukwepa maisha halisi ya Mtanzania na ku-copy tamaduni za kigeni na hali hiyo hutufanya kutofikia malengo na kutoweza kufika mbali zaidi na la mwisho kuthamini vipaji na uwezo binafsi na kusahau elimu nadhani tukienda shule tunaweza kulisukuma gurudumu hili la Tasnia ya filamu na kufika mbali, sababu kubwa ya kuwepo kwa WORKSHOP za filamu sasa ambazo mara kwa mara zinazoingia hapa nchini ni kwa lengo la kupata elimu zaidi juu ya uandaaji wa filamu na kuelewa zaidi misingi ya kufanya kazi iliobora.
TUKIIFATA ELIMU TUTAFIKA...