Ni baada ya muda mufupi kupita Msanii ambae anafanya vizuri katika anga ya muziki wa miondoko ya Hip Hop ndani na nje ya Nchi Ambwene Yesaye akifahamika zaidi kama AY baada ya kulalamika sana kwenye mitandao ya kijamii juu ya watu ambao wanatumia namba zake katika kumfanyia wizi.
Jana siku ya Jumamosi majira ya saa Tisa alasiri maeneo ya Coco Beach Masaki, AY alionekana akiwa na Msanii mwenzie Fareed Kubanda almaarufu Fid Q huku wakiwa na jamaa wapatao watatu wengine, wakiwa jumla ya watu watano ambao wameonekana wakiwa wameegesha gari zao Harrier
na nyingine ambayo haikuweza kutambulika kwa urahisi.
Walionekana kumshusha kijana mmoja ambae wamemfunga pingu huku wakimuuliza maswali aweze kuwataja ni nani ambae aliweza kutoa Fedha za Msanii huyo AY huku Fid Q nae anaonekana kuwa mwenye ghadhabu sana na huyo kijana pengine nae alishapigwa changa na hao watu.Tukio hili likiendelea Fid Q na AY wakiwa wanamrekodi jamaa huyo wakati akiwa anatoa maelezo na kuwataja jamaa ambao waliokuwa wanahusika na mchezo mchafu ambao walioweza kuwafanyia wasanii hao.
Zoezi hilo lilichukua muda wa saa moja na nusu, hatimae kumchukua kijana huyo na umuingiza kwenye gari na kuondoka nae.
Hii ni picha ambayo iliweza kunaswa wakati tukio likifanyika. |