Sunday, December 1, 2013

R.I.P PAUL WALKER

Muigizaji wa Marekani, Paul Walker pichani aliyekuwa akiigiza kwenye filamu ya Fast & Furious amefariki dunia kwa ajali ya gari California.

Msemaji wake ametoa taarifa ya kifo chake kupitia Facebook kudai Walker, 40, alikuwa amebebwa kwenye gari ya rafiki yake iliyopata ajali Kaskazini mwa jiji Los Angeles. Alikuwa akienda kuhudhuria tukio la utoaji misaada.

Paul aliigiza kwenye series za filamu ya Fast and The Furious ambazo hadi sasa ni sita. Walker pia ameigiza kwenye filamu iitwayo Hours, ambayo itazinduliwa mwezi huu. Mamlaka zimesema waliikuta gari hiyo ikiwaka moto na watu wawili waliokutwa kwenye gari hiyo walikutwa wamekufa tayari


Imeandikwa na Ammar Ruweih












  • Paul Walker
    Actor
    Paul William Walker IV was an American actor. He became well known in 1999 after his role in the hit film Varsity Blues. However, he is perhaps best known for starring as Brian O'Conner in The Fast and the Furious film series.
  • BornSeptember 12, 1973, Glendale, California, United States



  • Height6' 2" (1.88 m)