
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Manzese waanguka ovyo huku ikisemekana kuwa ni nguvu za giza zikiendelea mahala hapo.
Tukio hilo lilotokea majira ya saa nne asubuhi baada ya Mwanafunzi mmoja ghafla kuanza kupiga kelele darasani huku masomo yakiendelea, wakati anatolewa nje mwanafunzi huyo ndipo wanafunzi wengine walipoanza kuanguka ovyo shuleni hapo na kuendelea kupiga kelele kwa kijibizana.
Wakati tatizo likiendelea kwa wanafunzi hapo ilikuwa ni ngumu kuweza kutambua ni kitu gani kimewakumba wanafunzi hapo zaidi ya kufikiriwa kuwa kuna nguvu za giza ambazo zilikuwa zikiendelea mahala hapo.
Wanafunzi walikuwa wakianguka ovyo na kushindwa kujizuia huku wakipiga kelele na kuongea vitu ambavyo ilikuwa ni ngumu kuweza kuwaelewa yaani lugha ambayo haikuweza kueleweka, katika kelele hizo zikiendelea inasemekana kuna sauti nyingine ambazo zilikuwa zikisikika kutokea kwenye miti kama kujibizana na wanafunzi hao.
Viongozi wa dini zote mbili waliweza kuwepo katika eneo hilo na kuonesha ushirikiano katika tatizo hilo ambalo limewakuta wanafunzi hao, huku muda ukizidi kwenda na wazazi nao waliweza kujitokeza kwa wingi katika kuangalia watoto wao ilikuhakikisha usalama wao kutokana na taarifa mbaya ambayo ilioweza kusambaa kwa muda mfupi.
Hali inasemekana huwa inatokeaga katika siku za jumatato na si kwa Wanafunzi wengi kiasi hiki, ila leo imekuwa ni kitu tofauti sana na cha ajabu katika shule hiyo kwa tukio hilo kuangukia siku ya jumanne na Wanafunzi wengi sana zaidi ya 30 kuanguka ovyo na kupiga kelele huku wakiongea lugha isiyoweza kutambulika kirahisi.