Hali mkoani Mtwara, kusini ya Tanzania, inaendelea kuwa ya wasiwasi kufuatia ghasia za hapo majuzi kupinga uamuzi wa serikali kutaka kujenga bomba la kusafirisha gesi kutoka eneo hilo kuelekea Dar es Salaam.
Mapema, Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, aliliambia Bunge la nchi hiyo kwamba serikali imelazimika kutuma wanajeshi kutuliza hali, na sasa Waziri huyo anaripotiwa kuwapo Mtwara kutulizanisha hali
Saumu Mwasimba amezungumza na mwandishi wa habari wa Redio Safari, Bryson Mshana, juu ya kinachoendelea katika mkoa huo wa sasa.
Mwandishi: Saumu Yusuf
Mhariri: Mohammed Khelef
Mhariri: Mohammed Khelef
