.jpg)
NA RENATHA MSUNGU
Washiriki wa shindano la urembo la kitongoji cha Tabata 'Miss Tabata 2013' watatembelea mbuga ya wanyama ya Mikumi iliyoko mkoani Morogoro ifikapo Jumapili imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shindano hilo, Godfrey Kalinga alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kukuza utalii wa ndani na kuwapa warembo fursa ya kujua vivutio vilivyomo kwenye mbuga hiyo.
“Hii siyo mara yetu ya kwanza kuwapeleka warembo wetu mbugani, tumekuwa tukifanya hivyo kila mwaka,” alisema Kalinga.
Kalinga alisema kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na kampuni ya CXC Africa na baada ya kurejea jijini washiriki hao wataendelea na mazoezi ya kujiandaa na shindano hilo litakalofanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Aliwataja wadhamini wa shindano hilo ni pamoja na gazeti la NIPASHE, Redd's, Dodoma Wine, Vayle Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, CXC Africa, Break Point na Saluti5.
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano hilo linaloandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts ni Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbalo (19), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Musa Kitereja (19), Rehema Kihinja (20), Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23), Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20), Caroline Sadiki (20) na Suzan Daniel (18).
Warembo watano wa juu watachaguliwa kushiriki shindano ya Kanda ya Ilala na baadaye fainali za taifa za Redd's Miss Tanzania.
Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.