Monday, May 20, 2013

Jeshi la Nigeria lauwa wanachama wa Boko Haram


Majeshi ya Nigeria yakipiga doria
Majeshi ya Nigeria yakipiga doria
Jeshi la Nigeria linasema limeuwa wanamgambo 14 wa kundi la Boko Haram na kuwakamata wengine 20 Jumapili. Jumanne iliyopita rais wa Nigeria Goodluck Jonathan aliamrisha kupelekwa kwa malefu ya wanajeshi upande wa kaskazini mwa nchi kupambana na wanachama wa Boko Haram,kundi la wanamgambo ambalo linalaumiwa kwa kusababisha  vifo vya maelfu ya watu katika muda wa miaka minne iliyopita.

Lakini kufikia Jumapili Jeshi lilisema wanamgambo hao 24 wa Boko Haram walikuwa wameuawa na wengine 85 kukamatwa. Baadhi ya wachambuzi wanahofu kuwa jeshi, ambalo makundi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu  yameshtumu kwa mauaji ya kiholela na ukiukwaji mwingine, huenda likatenga watu kwa kuuwa raia pale linapowasaka wanachama wa Boko Haram.

Mwandishi wa VOA katika mji wa Maiduguri, kitovu cha mapambano kati ya jeshi la Nigeria na wanamgambo hao anasema wakaazi wengi wameathiriwa na tangazo la kutotoka nje la saa 24.Lakini wengine wana maoni kuwa pambano hili litafanikiwa kuleta amani katika ukanda huo ikiwa wanajeshi wataheshimu raia.

Operesheni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram iliamrishwa na rais baada ya ghasia  kuongezeka katika miezi ya karibuni. Maafisa wanasema Boko Haram ambalo linasema litataka kushinikiza sheria kali za Kiislam Sharia na kukomboa  wanachama wake waliofungwa jela