Monday, May 20, 2013

JADEN SMITH AJA NA AFTER EARTH

Ni mtoto mwenye umri wa miaka 14 ambae alipata umaarufu sana kupitia filamu ya KARATE KIDS Jaden Smith.

Natumai wengi mpaka hapo watakuwa wameshamuelewa vizuri kijana huyu ambae ni mtoto wa Will Smith.

Ndani ya Hollywood marekani imepelekea kuwashandaza wengi sana ambao wapo katika kuandaa filamu mbalimbali na zinazotamba hapa Duniani kutokana na alichokifanya Jaden katika filamu hiyo mpya ambayo ameshirikiana vyema na Baba yake Will Smith.
Director M. Night Shyamalan ambae alikuwa akiisimamia vyema filamu hiyo pia Mwandishi katika filamu ya After Earth wakati inaandalia aliweza kusema kuwa, Jaden ni kizazi ambacho kinakuja kushangaza ulimwengu katika upande wa filamu za mapigano "Action" au Martial Arts kitaalamu zaidi kutokana na umri wake mdogo.

Wakati wa maandali ya filamu hiyo ya After Earth muongozaji huyo alionekana akiwa hana kazi ngumu katika kumuongoza kujana huyo mdogo kutokana na uwelewa na kuwa makini sana tofauti kama inavyokuwa kwa waigizaji wengine wakubwa.

Ni filamu mpya ambayo inatarajiwa kutoka ndani ya mwaka huu miezi ya karibuni huku ikiwa tayari matangazo yakiwa yameweza kuachiwa katika mitandao mbalimbali tangu mwezi tar 9 mwezi huu.

AFTER EARTH.




Washiriki katika AFTER EARTH
Will Smith...
Jaden Smith...
Zoë Kravitz...
Senshi Raige
Isabelle Fuhrman...
Rayna
Kristofer Hivju...
Security Chief
Sophie Okonedo...
Faia Raige
David Denman...
Private McQuarrie
Glenn Morshower...
Commander Velan
Lincoln Lewis...
Bo
Faron Salisbury...
Sacha Dhawan...
Jaden Martin...
Jim Gunter...
Pakers
Chris Geere...
Navigator
Darrell Foster...
Ranger Instructor