Friday, May 17, 2013

Dortmund yachimba mkwara kwa Bayern


ARCHIV - Bayern Münchens Trainer Jupp Heynckes (r) und Trainer Jürgen Klopp vom BVB lachen am 19.11.2011 vor dem Spiel Bayern München - Borussia Dortmund. Jupp Heynckes erwartet beim Mega-Hit zwischen Borussia Dortmund und dem FC Bayern München ein Fußball-Fest für alle Anhänger. Foto: Frank Leonhardt dpa/lby/lnw (zu dpa 0271 vom 10.04.2012 ) +++(c) dpa - Bildfunk+++

MICHEZO

Dortmund yaionya Bayern kabla ya fainali

Zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya Fainali ya kukata na shoka ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uwanjani Wembley jijini London, mengi yanaendelea kufanywa ikiwa ni sehemu ya matayarisho ya dimba hilo.
Mkufunzi wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp amesema ana matumaini kwamba timu yake inaweza kuizidi nguvu Bayern Munich na kumaliza safari yao ya kujiondoa kutoka maisha ya kufilisika iliyoanza mwaka wa 2005.
Jurgen Klopp anasema safari ya kuelekea uwanjani Wembley imekuwa hadithi ya kuvutiaJurgen Klopp anasema safari ya kuelekea uwanjani Wembley imekuwa hadithi ya kuvutia
Dortmund watapambana na Bayern katika uwanja wa Wembley mnamo Mei 25 kwa ubingwa huo wa Ulaya, ikiwa ni miaka minane baada ya kuomba mkopo wa euro milioni mbili kutoka kwa mahasimu wao hao Bayern ili kuwalipa mishahara wachezaji.
Klopp anasema kama watashinda, hawatakuwa timu bora ulimwenguni, lakini watakuwa wameipiku timu bora ulimwenguni kwa sasa. Hata hivyo amekiri kuwa mabingwa hao wa msimu huu wa Bundesliga Bayern, wanastahili kupigiwa upatu katika kile kitakachokuwa ni Fainali ya kwanza kuwahi kuchezwa na vilabu viwili vya Ujerumani. Na bila shaka Kansela Angela Merkel amedhibitisha kuwa atahudhuria fainali hiyo katika uwanja wa Wembley ili kuwa sehemu ya historia. Ijapokuwa amekataa kuitaja timu atakayoishabikia kati ya hizo mbili.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu