TAMTHILIYA YA HIDDEN SECRET
Tamthiliya mpya na kusisimua ambayo iko katika maandalizi mazuri kwenye suala zima la kiufundi namaanisha huko kwa wenyewe ambao wanashughulikia kutaka kukamilisha.Ni HIDDEN SECRET Tamthiliya ambayo imejawa na visa mbalimbali Mapenzi, Visasi, Ukatili na mambo mengi tu ambayo yameizunguka dunia katika kila kona.
Kampuni ya PLAN B SOLUTION LTD ni kampuni ambayo inasimamia shughuli nzima ya Tamthiliya hii ya HIDDEN SECRET ikiwa inafanywa ndani ya ofisi zao zilizopo maeneo ya Sinza Mori. Mpaka sasa katika maandalizi hayo huku wakiwa wanaendelea na kuandaa kazi hivyo wanawaeleza Wadau na Wapenzi wa kazi za Filamu Tanzania na Nchi za jirani na mbali kuwa wakae tayari kwa Tamthilia itakayowajia muda si mrefu kwani mpaka sasa wamefanikiwa kuchukua Episod zipatazo 25 na Tamthiliya nzima ina Episod 48 hivyo tegemea kupata kitu kizuri kutoka katika Tamthilya ya HIDDEN SECRET.Kampuni ambayo inatengeneza Tamthiliya ya HIDDEN SECRET inapenda kuwatangazia pia kwa wale ambao wanatafuta nafasi za kushiriki katika Tamthiliya hii wawe tayari watatoa siku na tarehe ambazo watahitaji Wasanii na kuwafanyia majaribio na kuingia katika mchakato wa kushiriki katika tamthiliya hii. Ni moja ya lengo la kutaka kuinua na kutoa nafasi kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kuonekana huku wakiwa wanauwezo mzuri wa kuigiza baada ya hapo watakutana na Ma-Director ambao ni vijana wadogo wenye uwezo wa hali ya juu katika Uongozaji wa Filamu Tanzania pamoja na wapiga picha wazuri ambao wamepata taaluma hiyo na ni sehemu mojawapo katika kutoa elimu kwa wasanii wachanga juu ya ufanyaji wa filamu na maandalizi kwa ujumla ili kuja kuepuka usumbufu kwasababu kuna vitu vingi wasanii huwa hawavielewi pindi wanapofika katika eneo la kazi.
Kwasasa habari zilizokuwepo tu ni gumzo la jiji kwa Tamthiliya hii ya HIDDEN SECRET kabla ya kukamilika lakini Wadau wameshapata fununu na kujua ndani ya Kampuni ya PLAN B kuna dhahabu ambayo inaandaliwa kwaajili ya watazamaji wa kazi za filamu kuja kupata burudani ya kutoka katika Tamthiliya hiyo.
HIDDEN SECRET IKO NJIANI.....

