Sunday, December 23, 2012

HII NI HABARI YA KUFUNGIA MWAKA KWENYE MAMBO YA FASHION!!!!



Super Model in Tanzania

Tukiwa tumebakiza siku chache katika kuuga mwaka wa 2012 na kuukaribisha mwaka mpya kabisa, Leo habari iliokuwepo ni ya Yule kijana Mtanashati na mwanamitindo mahiri Nchini Tanzania Lota Mollel ambae amekuwa akifanya shoo mbalimbali na wengi wamekuwa wakimzoea katika shoo za Swahili Fashion Week leo amefunguka na kusema...
"Kwanza namshukuru Mungu, Pili nashukuru sana kwa kunipa support kubwa ambayo nimepata kwa Watanzania wenzangu na sehemu nyinginezo ambapo wanaweza kuniona na kuielewa kazi yangu, juu ya huu mwaka sina mengi ya kusema ila nafurahi sana kuwa Mimi ndie Model ambae nimefanya shoo nyingi sana katika mwaka huu kuliko wote hiyo ni nafasi pekee ambayo najivunia kwasababu wengi huwa wanatafuta nafasi hiyo lakini inakuwa ngumu. Siri kubwa ni kujituma na kuipenda kazi yako mwisho nidhamu ndio kila kitu mahala popote ukiwa hivyo naimani utafika mbali"
Hayo ni maneno ya Lota Mollel ni mwanamitindo ambae amevunja rekodi kwa kufanya shoo nyingi sana hapa Nchini kwetu Tanzania....Hongera Brother!!!!!