Thursday, December 27, 2012

DIRECTOR WA MASUMBUKO ATEMA CHECHE...









Ni baada ya muda mfupi kukamilika kwa filamu ya dakika 5 ya MASUMBUKO Director wa filamu hiyo amekuwa katika tofauti ili kutaka kuweka mambo sawa juu ya filamu hiyo kuwepo katika filamu mbalimbali za kimataifa hapa nchini.
Katika Tasnia ya Filamu Tanzania mara nyingi wachache ambao huwa wanaangalia katika kujitangaza katika mataifa mengine au soko la Kidunia kwenye Tasnia hii lakini mbali na hayo kwa kipindi hiki wadau na wapenzi wa filamu za nyumbani wameeanza kupata uelewa kutokana na kazi nzuri ambazo zinafanywa na wachache hususani wale ambao wanaonekana kuudhuria WORKSHOP mbalimbali ili kupata elimu zaidi katika maswala ya filamu kwa ujumla.

Director wa filamu hii ya MASUMBUKO Ally Kasongo Ram baada ya kupata nafasi ya kupata Form ambayo itakayomfanya filamu yake hiyo kwenda katika mashindano Kisiwani Zanzibar kwenye Tamasha la ZIFF [Zanzibar International Films Festival] aliweza kuongea mengi sana lakini yote katika kuamasisha wadau na waandaaji wa filamu kuzingatia vitu fulani ili katika kufanikiwa kufanya kazi nzuri na kujitoa katika kushiriki kwenye matamasha mbalimbali ambayo yanahusiana na filamu ili kupata taaluma na kufahamiana na watu katika kubadilishana mawazo kutokana na taaluma amabazo wanazo wenzetu katika kupiga hatua sana kwenye Dunia ya filamu.
Haya yalikuwa machache kutoka kwa Dir. Ally Kasongo Ram.

"Leo hatua ambayo tukonayo si hatua ya kuichezea na pia kujiamini sana kwani tunahitajika kujitangaza kidunia zaidi ili kuweza kufaika katika soko la filamu la kimataifa mfano kama Nchi za wenzetu walio jirani Nigeri, Ghana, South Africa n.k kiasi ambacho wanaonekana kupiga hatua sana na kufahamika katika soko la kimataifa. Inanisikitisha kusikia kuwa Nchi za Ulaya katika maktaba zao hakuna Filamu za Kitanzania zikiuzwa ila zaidi ya Ghana, Nigeri, South Africa n.k na kila DVD moja huuzwa kwa Euro 10 hadi 8 ambayo ni kiasi cha Shilingi 20,000 kwa kadirio la chini, inafaa kujiuliza maswali kwani Nchi za Ulaya hakuna Watanzania? na kwanini kazi zetu hazipo katika maktaba zao?. Lengine la kushangaza Ma-pirus hawapo Tanzania tu bali hata nchi za ulaya wapo ni kwa Watanzania ambao wanaishi Ulaya huwa wanafanya biashara hiyo kwa wenyewe kwa wenyewe kutokana hakuna pakuzipata kwenye maktaba zote za ulaya bali kwa Watanzania ambao wanaoishi huko huagiza kwa watu wao ambao wako huku na kutumiwa na kweli hufanya biashara kwa kiasi kikubwa na bei ni kawaida kama huku tunavyouza. Nina imani tukiwa tunashiriki katika matamasha mbalimbali tutapata elimu ya kutosha na njia mbadala katika kufanya kazi zetu kwa Taaluma zaidi na kutimiza ndoto zetu katika kujitangaza Kimataifa"

Tasnia ya Filamu Tanzania inakua, kilichokuwepo ni kukubali matokeo kuwa elimu ndio kila kitu pia Wadau na Waandaaji wa Filamu wanatakiwa kuudhuria Matamasha mbalimbali katika kupata elimu na uzoefu zaidi ili kuweza kufanya kazi zilizokuwa Bora na Nzuri ili zikubalike katika mataifa mengine kama kazi za wenzetu wa nchi zilizotuzunguka.